Tarehe ya kuanza kutumika: 27 Septemba 2026.
1. Madhumuni ya website
Website hii hutoa taarifa za jumla kuhusu FKF na huduma zinazopangwa. Taarifa ya website pekee si idhini, mkataba wala ahadi ya kutoa mkopo au huduma.
2. Maombi na KYC
Maombi rasmi yanafanyika kupitia portal na yanaweza kuhitaji KYC, nyaraka, tathmini na idhini kulingana na bidhaa. FKF inaweza kuomba ufafanuzi au kukataa ombi kulingana na vigezo vinavyotumika.
3. Kikokotoo
Matokeo ya kikokotoo ni makadirio kwa kutumia taarifa ulizoingiza. Kiasi, gharama na ratiba ya mwisho ni ile iliyo kwenye nyaraka rasmi zilizokubaliwa.
4. Malipo
Tumia rejea na njia rasmi zilizotolewa ndani ya portal au nyaraka za FKF. Usilipe kwenye namba binafsi ya mfanyakazi. Hakiki risiti baada ya muamala.
5. Matumizi yanayokubalika
Hairuhusiwi kujaribu kuvunja usalama, kuingiza taarifa za uongo, kuiga website, kutumia nembo bila ruhusa au kutumia huduma kwa udanganyifu.
6. Mabadiliko
Maudhui yanaweza kusasishwa wakati maandalizi na huduma zinavyoendelea. Toleo jipya litaonyesha tarehe iliyosasishwa.
7. Mawasiliano
Maswali kuhusu masharti haya yatumwe kwa helpdesk@fkf.co.tz.